Thursday, June 18, 2009

Bajeti imejaa 'usanii'- Lipumba

Chairman wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba amesema Bajeti ya Serikali iliyowasilishwa bungeni wiki iliyopita na Waziri wa Fedha na Uchumi, Bw. Mustafa Mkulo imejaa usanii

Akiongea kwa kujiamini,Mh. huyo alisema bajeti hiyo imewasilishwa 'kisanii' kutoka chama cha 'kisanii' kinachoongozwa kwa 'usanii' mkubwa.

"Bajeti hiyo hakidhi mahitaji ya wananchi na inalenga kuwadidimiza na kuongeza umasikini nchini" alisema Prof Lipumba.

Alisema usanii kwenye bajeti hiyo ulianzia pale Serikali ilipotangaza kufidia hasara waliyopata wanunuzi wa mazao kwa msimu uliopita wa 2008/09 hasara hiyo ni kiasi cha sh. bilioni 21.9

Alisema Serikali italipia hasara hiyo ambayo imetokana na kushuka ghafla kwa bei ya mazao ya Tanzania katika soko la dunia wakati fedha hizo hazioneshwi katika vitabu vya bajeti.

Aliongeza kuwa hotuba ya Rais Kikwete aliyotoa mjini Dodoma hivi karibuni ya bajeti imeeleza kuwa serikali itatoa udhamini kwa mikopo inayofikia sh. bilioni 270 .


Alisema kuna hatari kuwa serikali inajiingiza kudhamini madeni ambayo hatimaye hayatolipwa na wanaodhaminiwa na kujiongezea mzigo wa madeni kwa nini madeni haya yadhamiminiwe kwa miaka miwili na sio mmoja?


"Wasi wasi wangu ni kwamba imeamua wadhaminiwe kwa miaka miwili ili watakaodhaminiwa wachangie kwenye kampeni za CCM,"alisema Prof. Lipumba.

Kikwete azingirwa

• Hoja za maaskofu, wabunge zamuelemea


na Waandishi Wetu




RAIS Jakaya Kikwete, sasa anaonekana kuzingirwa kila upande na makundi mbalimbali ya kijamii, ambayo hayaridhishwi na mwenendo wa mambo katika serikali anayoiongoza kiasi cha kuanza kutilia shaka maamuzi mazito yaliyofikiwa.

Hali hiyo ya manung’uniko, kuinyoshea serikali kidole na kumlenga Kikwete binafsi pasipo kumtaja moja kwa moja, imedhihirika tangu Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkullo, asome hotuba yake ya Bajeti ya Serikali ya mwaka wa Fedha wa 2009/2010, Alhamisi, wiki iliyopita.

Hotuba hiyo ya bajeti ambayo inapingwa na wabunge wengi waliokwishaijadili, viongozi wa dini, viongozi wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NG’Os), pamoja na wanaharakati, inamuweka Rais Kikwete katikati ya upinzani mkali kutoka kwa watu anaowaongoza na inatoa ishara ya kuwapo mtikisiko mwingine mkubwa serikalini.

Katika hali inayoonyesha kuishiwa uvumilivu kwa baadhi ya wabunge wa CCM, ambao hawako karibu na wateule wa Kikwete serikalini, sasa wameanza kuhoji miradi tata inayotekelezwa kinyume cha taratibu na wasaidizi wake.

Moja ya miradi tata inayotekelezwa kinyume cha taratibu za serikali uliotajwa bungeni juzi, ambao unamgusa moja kwa moja Rais Kikwete, ni ule wa ujenzi wa barabara ya Chalinze – Segera, unaodaiwa kuanza kutekelezwa kabla ya kuidhinishiwa fedha katika bajeti ya serikali. Mradi huo unapita katika eneo ambalo ni nyumbani kwao na Rais Kikwete.

Mradi huo ambao unaonyesha dalili za kuwapo upendeleo katika usambazaji huduma za maendeleo hapa nchini, iwapo utathibitika kuwa unatekelezwa kinyume cha taratibu, unaweza kumchafua Rais Kikwete kiasi cha kumfanya aonekane kuwa miongoni mwa viongozi wanaopendelea maeneo ya kwao katika utoaji huduma za jamii na maendeleo.

Tayari Spika wa Bunge, Samuel Sitta, juzi aliitaka serikali kutoa maelezo ya suala aliloliita zito sana la kuanza kutekelezwa kwa mradi huo ambao utakuwa unatumia fedha za bajeti ambayo haijapitishwa wala kujadiliwa.

Spika Sitta alitoa agizo hilo kwa serikali baada ya Mbunge wa Nzega, Lucas Selelii (CCM) kutaka mwongozo wake kuhusu mahali ambako serikali imepata mamlaka ya kuanza kutumia fedha za bajeti kabla hazijapitishwa.

Selelii, mmoja wa wabunge ambao wamekuwa wakilalamika kuandamwa na mafisadi majimboni kutokana na harakati zao za kupambana nao, alikwenda mbali zaidi kwa kulishambulia Baraza la Mawaziri kuwa limejaa watu wabinafsi, wenye roho mbaya, wenye lengo la kutaka kukwamisha baadhi ya wabunge na akamuomba Mungu awalaani.

Mbunge huyo, alikuwa miongoni mwa wabunge wa mwanzo kuichangia hotuba hiyo huku akionekana kuwa mwiba mkali zaidi kwa serikali na Baraza la Mawaziri, jambo linalotafasiriwa na baadhi ya wachambuzi wa mambo kuwa ni mwanzo wa vita ya wazi ya kuhakikisha anapambana kubaki kwenye kiti chake cha ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwakani.

Baadhi ya wadadisi wa mambo waliozungumza na Tanzania Daima Jumatano, wanaielezea kauli ya Selelii dhidi ya mawaziri kuwa iliyokuwa ikimgusa moja kwa moja Rais Kikwete, ambaye kikatiba ndiye Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri.

Hoja hizo za awali bungeni zilikuja siku chache tu baada ya maaskofu kadhaa wa makanisa makubwa nchini ya Katoliki, Anglikana na Lutheran kuelezwa kusikitishwa na hatua ya Serikali ya Kikwete kufuta misamaha ya kodi kwa mashirika ya dini.

Baadhi ya maaskofu hao, akiwamo Benson Bagonza wa Kanisa la Kilutheri, Karagwe walifikia hatua ya kusema kuwa walikuwa wakikusudia kuishitaki serikali kwa waumini wao katika mimbari, hatua ambayo iwapo itatekelezwa inaweza kusababisha athari za kisiasa wakati wa uchaguzi mkuu wa mwakani.

Mwenendo huo wa kutoridhishwa na bajeti hiyo ya serikali, uliendelea kuonekana hata jana wakati Bunge lilipokuwa likiendelea kuijadili, huku wabunge wakionyesha dhahiri kuweka kando itikadi za vyama vyao.

Akichangia hotuba ya Waziri wa Fedha na Uchumi, Mkulo bungeni jana, Mbunge wa Kishapu, Fred Mpendazoe (CCM), alisema kukosa umakini kwa viongozi kumeisababishia nchi matatizo makubwa na kuwafanya wananchi wake kuwa masikini.

“Ashakum si matusi, lakini mawe yaliyo baharini hayawezi kusikia kilio cha mtende ulio jangwani, wakati watu wanapiga vita ufisadi, wengine wanakejeli,” alisema Mpendazoe.

Alihoji inakuwaje mpaka sasa watu waliohusika katika kuingiza nchi katika mikataba mibovu, ukiwamo wa Kampuni ya Richmond hawachukuliwi hatua za kisheria na serikali inaendela kuwatengea bajeti kila mwaka.

“Watendaji wa serikali ambao wameiingiza nchi katika mikataba mibovu, ikiwamo ya Richmond, reli na Kiwira kwa nini hawachukuliwi hatua mpaka sasa? Wananchi wanataka kufahamu. Kutochukua hatua dhidi ya uovu maana yake ni kuubariki, hivyo serikali inapokuwa haichukui hatua dhidi ya ufisadi na mafisadi maana yake inabariki,” alisema Mpendazoe.

Pia aligusia suala la kampuni ya upatu ya DECI kwa kueleza kuwa wananchi walijiunga katika kampuni hiyo baada ya kutokuwa na mbadala na kuongeza kuwa, riba za mikopo katika benki zimekuwa kubwa na serikali imekuwa haifanyi jitihada za kuwasaidia wananchi.

Aidha, mbunge huyo alishangazwa na kuwapo kwa utiriri wa Wachina na Wakorea jijini Dar es Salaam, ambao wanafanya kazi zinazoweza kufanywa na Watanzania huku wenyewe wakibaki bila ajira.

Mbunge wa Maswa, John Shibuda (CCM), yeye alihoji ni lini Watanzania watashika hatamu ya kuendesha mashirika mbalimbali yaliyopo nchini.

Alitoa mfano wa Shirika la Reli kwa kueleza kuwa awali lilipokuwa likiendeshwa na Watanzania, lilikuwa likifanya vizuri, lakini tangu wamepewa wawekezaji wa kutoka India, limekuwa na matatizo.

“Naomba mawaziri mtueleze hivi mnatupeleka wapi Watanzania? Mkataba wa TRL, TICTS… uzalendo wenu utapimwa vipi? Tumechoka, tunataka mtekeleze ilani ya chama vizuri,” alisema Shibuda.

Alimgeukia pia Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na kumtaka kuondoa shughuli za kutengeneza vitambulisho vya taifa katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa vile hakuna kinachoendelea katika utekelezaji wa kazi hiyo bali malumbano.

“Vitambulisho hivi vinaweza kuliingizia taifa mapato makubwa, kwani kuna watu wanaostahili kulipa kodi karibu milioni 18, tukivitumia vizuri vitatusaidia…lakini imeshindikana, wakati wa kubebana umepita, vitambulisho hivyo viondolewe,” alisema Shibuda.

Aidha, aliwatahadharisha vingozi kuhusu ugawanyaji sawa na ‘keki ya taifa’ na kutaka kutokuwapo kwa upendeleo katika maeneo wanayotoka viongozi, na akahitimisha hoja yake kwa kusema alikuwa ameahirisha kuiunga au kuipinga bajeti hiyo akisubiri majibu kutoka kwa Waziri Mkulo.

Mbunge wa Mkanyageni, Mohamed Mnyaa (CUF), aliwamtaka Waziri wa Fedha na manaibu wake kujiuzulu kutokana na tamwimu za hasara iliyopata serikali kutokana na rasilimali za nchi kunufaisha nchi nyingine. Alitoa mfano wa rasilimali ambazo zinanufaisha nchi za jirani kuwa ni magogo, ng’ombe na alizeti.

“Juzi, Mheshimiwa Sakaya (Magdalena) alipouliza swali hili, Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi alisema hana takwimu. Je, kwa hii nilivyotaja serikali haijapata hasara? Naomba waziri na manaibu wake wajiuzulu kama hawana takwimu... huu si wakati wa kuoneana haya,” alisema Mnyaa.

Aidha, alisema pamoja na serikali kusema katika bejeti hiyo kuwa ‘kilimo kwanza’, lakini mafanikio katika sekta hiyo hayatapatikana bila ya kuwapo kwa umeme katika maeneo mengi nchini.

Alihoji kitendo cha serikali kupunguza bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini huku safari za ndani na nje ya nchi zikitengewa sh bilioni 34.6.

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Elisa Mollel (CCM), alisema ubaguzi unaoendelea wa kupeleka maendeleo kwa baadhi ya maeneo nchini si mzuri. Alisema wananchi wa jimbo lake mpaka sasa hawana maji, lakini mabomba ya maji yamepita katika jimbo hilo na kupeleka huduma hiyo katika Jimbo la Monduli.

“Sina ugomvi wa watu wa Monduli, lakini si vema inavyofanyika, wananchi wa Arumeru Mashariki mpaka sasa hawana huduma ya maji,” alisema.

Naye Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo (CHADEMA), alisema Rais Kikwete amepotoshwa kwa kuelezwa kuwa visa ya watalii imepunguzwa kutoka dola 100 hadi dola 50 na kusema kilichopunguzwa ni kiingilio cha watalii.

Alisema mgeni yeyote anayeingia nchini hutozwa visa ya dola 50 na kuongeza kuwa hata kama serikali imepunguza kiingilio cha watalii bado havivutii, kwani Kenya wanatoza dola 25.

Pia aliomba serikali kutafakari upya kufuta msamaha wa kodi kwa mashirika ya dini na kusema kama kweli kuna watu waliotumia vibaya misamaha hiyo serikali iwashitaki.

“Lakini kwa kuwa mpaka sasa hakuna mtu aliyeshitakiwa, naamini hakuna aliyetumia vibaya misamaha hiyo,” alisema Ndesamburo na kuongeza kuwa, huduma inayotolewa na mashirika ya dini katika jamii ni muhimu.

Kwa upande mwingine, viongozi wa dini nao wamekwishaeleza kutokubaliana na uamuzi wa serikali wa kutaka kulipia kodi baadhi ya vifaa vya kibiashara wanavyopatiwa kama msaada au wanavyonunua kutoka nje ya nchi.

Msimamo huo unawajumuisha viongozi wa dini zote kubwa hapa nchini na baadhi yao wamekwishaeleza kuwa iwapo serikali haitawasilikiza na kubadili uamuzi wake huo, basi hukumu yake itapatikana katika uchaguzi mkuu wa mwakani.

Viongozi hao wa dini wamekwishaeleza kuwa wanaandaa waraka wa kupinga uamuzi huo wa serikali na baadhi wamekwishaanza kutoa elimu kwa waumini ya jinsi ya kuchagua viongozi wanaofaa, jambo linaloashiria kuwa ni maandalizi ya mapema ya kuwaandaa waumini kutofanya makosa katika uchaguzi ujao.

Monday, June 15, 2009

MSINISEME”-ALI KIBA

Mpaka hivi sasa yeye ndio anashikilia rekodi ya msanii wa Bongo Fleva ambaye amefanya ziara ndefu ya kimuziki nje ya Afrika Mashariki.Hapa tunamuongelea kijana Ali Kiba ambaye jumamosi hii atakuwa Washington D.C katika muendelezo wa ziara zake.

Wakati anaendelea na ziara,Ali Kiba ameachia single yake inayokwenda kwa jina Msiniseme. Tofauti na nyimbo zake nyingi,hii imekaa kwa kuchezeka zaidi ndani ya club au sehemu yeyote ya kujirusha.



Lipo pia swali ambalo tumetumiwa na msomaji wetu mmoja.Anataka ufafanuzi kwamba Ali Kiba anatokea wapi.Ni Mkenya au Mtanzania? Anasema amesikia sehemu mbalimbali Wakenya wakisema Ali Kiba ni mtu wa kwao wakati anavyojua yeye Ali Kiba ni Mtanzania.

Kwa faida ya msomaji wetu na wengine wengi,tunavyojua sisi Ali Kiba ni mtanzania.Nyumbani kwao ni Kariakoo jijini Dar-es-salaam.

Viongozi wa dini wazidi kumkalia kooni Mkulo

Exuper Kachenje na Salim Said


VIONGOZI wa dini za Kiislamu na Kikristo jana waliendelea kumkalia kooni Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, licha ya kueleza kuwa ufisadi katika baadhi ya taasisi hizo ndio uliofanya serikali itangaze katika bajeti yake kuwa inazifutia msamaha wa kodi.


Akijaribu kutuliza viongozi wa dini waliokasirishwa na kitendo cha serikali kufuta misamaha ya kodi kwa taasisi za dini na mashirika yasiyo ya kiserikali, Waziri Mkulo alisema baadhi ya vyombo hivyo vimekuwa vikitumia vibaya misamaha hiyo na kwamba ameiagiza Mamlaka ya Mapato (TRA) kutoa orodha ya vitu ambavyo vitasamehewa kodi.


Aidha alisema vitu vyote vya huduma, ikiwa ni pamoja na vya hospitali na shule havitatozwa kodi na kwamba tayari ameiagiza TRA, kuandaa orodha ya vitu vyote vitakavyotozwa na vitakavyosamehewa ushuru. Katika hotuba yake ya Alhamisi, Mkulo alisema vitu ambavyo havitatozwa kodi ni vile vya huduma za kiroho tu.


Lakini viongozi wa dini walielezea kauli hiyo ya Mkulo kuwa haina msingi na kwamba angekutana kwanza na wadau kabla ya kutangaza kufuta misamaha hiyo kwenye bajeti yake ya mwaka 2009/10 aliyoisoma bungeni mjini Dodoma Alhamisi iliyopita.


Wakizungumza na gazeti hili jana, viongozi hao wa dini walisema uchafu na ukosefu wa maadili upo takriban katika kila sekta, lakini wakasema hiyo haifanyi wahusika wote wastahili kuadhibiwa na kufafanua kuwa Mkulo anaweza kutangaza taasisi za dini ambazo zimedanganya katika kupata misamaha ya kodi.


Askofu Msaidizi wa Kanisa Katokili Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Method Kilaini aliiambia Mwananchi jana kuwa kitu ambacho Mkulo na serikali yake walitakiwa kufanya ni kukutana na wadau na kuwaeleza uamuzi wao; mapungufu waliyoyaona pia kusikia maoni ya taasisi za dini.


"Kama kutangazwa majina ya wanaotumia vibaya misamaha, sisi hatuna shida atangaze tu," alisema.


Kilaini alisema: "Mkulo anapaswa kukutana na wadau na kuwafafanulia kuhusu hatua hiyo kabla ya TRA haijataja wale anaodai Mkulo wanaotumia vibaya misamaha hiyo.


Kama wabunge wamemwelewa kama sisi tulivyoelewa anategemea sisi tumwelewe vipi? Awaite wadau awafafanulie.


"Bado nasisitiza kuwa hatua hiyo si sahihi. Wabaya wapo kila mahali, lakini huwezi kutupa mtoto kwa sababu mkono wake umeingia maji machafu.


"Wanaovunja sheria wapo kila mahali huwezi kuhukumu wote kwa kosa la wachache. Katika taasisi za dini wapo wanaovunja sheria. Zipo taasisi hata makanisa yanayoanzishwa kwa lengo la kupata msamaha wa kodi na ilitakiwa serikali idhibiti hilo si kufuta kodi kwa wote."


Aliongeza kuwa ndani ya mfumo wa serikali kuna mapungufu na matatatizo mengi, akiyataja baadhi kuwa ni wizi wa fedha kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), majina ya walimu hewa na mengineyo.


"Ikiwa kasoro ya wachache, inahusisha wote basi walimu wangefutwa wote na pia serikali isingerudisha ruzuku kwa wafanyabiashara," alisema.


Kaimu mufti wa Tanzania, Sheikh Suleiman Gorogosi alisema kwa sasa hawawezi kuzungumza lolote hadi hapo waziri huyo atakapotoa orodha hiyo na baada ya wao kuichambua, ili kuona ni kwa kiasi gani imetoa nafuu kwa taasisi hizo au imezidi kuzikandamiza.


"Haya unauliza wakati orodha yenyewe haijatolewa; yeye si kafafanua; si kasema ameiagiza TRA kuandaa orodha hiyo na kuichapisha magazetini? Sisi tunaisubiri kwa hamu hiyo orodha yake," alisema Sheikh Gorogosi.


Alifafanua kuwa iwapo orodha hiyo itatoa unafuu kwa taasisi za dini, wao hawana tatizo. Lakini akaongeza kuwa ikiwa itazidi kuwakandamiza kwa kulazimisha ushuru hata kwa vitu vya huduma katika taasisi na mashirika ya dini, hawataikubali.


Naye Mchungaji John Magafu wa idara ya habari ya Jumuia ya Makanisa Tanzania (CCT) alisema kuwa taasisi za dini zinafanya kazi kwa uwazi, hivyo ni bora Mkulo akaweka wazi taasisi zinazotumia vibaya msamaha wa kodi kwa majina.


"Sisi tunafanya mambo kwa uwazi. Ili kuondoa utata unaotumika kuzikandamiza taasisi zote za dini, ataje wahusika wala si jambo la kututia hofu," alisema Mchungaji Magafu.


Alisema kimsingi kama Waziri Mkulo ana ushahidi, yupo huru kutangaza wale wanaotumia vibaya misamaha hiyo. Serikali isifanye kiini macho na kuaminisha wananchi kuwa mapato yake yanategemea zaidi taasisi na mashirika ya dini.


Katibu mkuu wa Kamati ya Kutetea Haki za Waislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda alisema hawataikubali orodha yoyote ambayo itataka vitu vya kutolea huduma katika taasisi na mashirika ya dini kutozwa ushuru.


Alisema Waislamu wanasikitika kuona hata misikiti inatozwa kodi wakati hakuna biashara yoyote inayofanyika ndani zaidi ya watu kuingia kufanya ibada na kusoma na baadaye kutoka.


Alisema suala la kutotozwa kodi kwa bidhaa na vitu vya huduma hususan vya kiroho, kiibada, hospitali na hata mashuleni ni haki ya waumini kwa sababu serikali imeshindwa kuwatosheleza katika huduma hizo.


"Kwa miaka mingi serikali imekuwa ikitunyanyasa kwa kututoza kodi katika vitu vya kiibada, kiroho na huduma, lakini kwa sasa hatutakubali kwa sababu ni haki yetu na tutaidai," alisema Sheikh Ponda.


Kauli za viongozi hao wa dini ni mwendelezo wa mjadala mkali ulioibuka hata kabla ya hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka 2009/10 iliyotolewa bungeni Alhamisi iliyopita baada ya kubainika kuwa taasisi za dini na zile zisizo za kiserikali zinafutiwa kodi.


Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe alisema: "Serikali imeonyesha udhaifu mkubwa katika msamaha wa kodi ya mafuta kwa kampuni za madini, kwani inataka kushauriana nao kwanza. Sasa ni kwanini haikushauriana na vingozi wa dini kabla ya uamuzi huo kama inavyotaka kwa makampuni ya madini?


"Ina maana kuwa serikali inathamini uwekezaji kuliko dini na shughuli za dini? Natambua kuna taasisi za dini zinatumia vibaya misamaha hii, lakini kwa nini serikali itoe adhabu kwa taasisi zote? Ni jukumu la serikali kudhibiti abuse (matumizi mabaya) hiyo."


Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, alielezea msamaha wa kodi ya mafuta ya petroli kwa kampuni za madini nchini umelikosesha taifa Sh181 bilioni toka uanze mwaka 2005.


"Msamaha huo ulitolewa wakati kampuni zote zikiwa tayari zina mikataba, hivyo kimsingi msamaha huo haupo kwenye mikataba ya madini ambayo serikali imeingia nayo," alisema Zitto.

Tuesday, May 26, 2009

Richmond, TICTS, TRL kutikisa Bunge

• Karamagi, Msabaha, Hosea, Mwanyika roho juu


na Deogratius Temba




HATIMA ya baadhi ya watuhumiwa waliohusishwa na kashfa ya kutoa zabuni kwa Kampuni ya kuzalisha umeme wa dharura ya Richmond inatarajiwa kujulikana katika mkutano wa Bunge la bajeti unaotarajiwa kuanza Juni 9 mwaka huu.

Kashfa ya zabuni ya Richmond ndiyo iliyomfanya aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na aliyekuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ibrahim Msabaha, kujiuzulu, jambo lililosababisha kuvunjwa na kuundwa upya kwa baraza la mawaziri.

Tangu kutokea kwa kashfa hiyo hadi sasa, hali ya upepo si salama ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), hasa baada ya kuibuka makundi mawili makubwa, moja likijinasibu linapinga ufisadi huku jingine likidaiwa kupambana na wale wote wanaoendesha vita dhidi ya ufisadi.

Miongoni mwa watuhumiwa waliotakiwa kuwajibishwa na serikali ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali Johnson Mwanyika, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Edward Hosea, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na aliyekuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ibrahim Msabaha.

Hatima ya watu hao itajulikana baada ya Bunge kupokea taarifa ya serikali kuhusu utekelezaji wa maazimio ya Bunge kutokana na hoja binafsi ya uuzaji wa nyumba za serikali, iliyowasilishwa bungeni na Mbunge wa Vunjo (CCM), Aloyce Kimaro na taarifa ya uamuzi wa serikali kuhusu mkataba wa Kampuni ya kimataifa ya kupakua na kupakia makontena bandarini (TICTS).

Aidha, pia Bunge litapokea utekelezaji wa serikali juu ya maazimio ya Bunge kuhusu Kampuni ya Richmond, taarifa ya serikali kuhusu uendeshaji wa Shirika la Reli nchini (TRL), na utaratibu wa ugawaji wa vitalu vya kuwindia na bei zake, ambao kisheria muda wake unaisha mwaka huu.

Mbali na taarifa hizo, pia serikali inatarajiwa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mapendekezo ya kamati maalumu ya rais, ya Nishati na Madini iliyokuwa chini ya Jaji mstaafu, Mark Bomani, na serikali itatoa taarifa juu ya ripoti ya hesabu za mashirika ya umma ambayo iliwasilishwa hivi karibuni.

Taarifa ya Bunge kupokea utekelezaji wa maazimio hayo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu shughuli zinazolikabili Bunge.

“Tunategemea baada ya kipindi cha maswali na majibu, na mjadala wa bajeti kumalizika, Bunge litapokea taarifa ya maazimio 23, ya Richmond, kuhusu uendeshaji wa Shirika la Reli (TRL) na TICTS,” alisema.

Alisema siku ya kwanza ya mkutano huo utafuatwa utaratibu wa kawaida wa kula kiapo cha uaminifu kutoka kwa mbunge wa Jimbo la Busanda, atakayechanguliwa leo, kufuatiwa na kipindi cha kawaida cha maswali na majibu, ambapo Juni 11, Waziri wa Fedha na Uchumi, atawasilisha taarifa rasmi ya hali ya uchumi nchini, na kufuatiwa na kuwasilishwa kwa hotuba ya bajeti siku hiyo jioni.

Alisema kwa mujibu wa kanuni ya Bunge namba 96(2), makadirio ya fedha za matumizi yatawasilishwa bungeni na Waziri wa Fedha na Uchumi kwa hotuba ambayo hutolewa kabla ya Juni 20 kila mwaka.

“Kwa kuzingatia makubaliano ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, bajeti za nchi wanachama kwa mwaka wa fedha wa 2009/10, zitasomwa siku ya Alhamisi Juni 11, 2009,” alisema Dk. Kashililah.

Pia alisema kwa mujibu wa kanuni 96(6), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Fedha na Uchumi pamoja na Kiongozi wa upinzani Bungeni, watapewa muda wa saa moja kila mmoja kuwasilisha maoni yao kuhusu hotuba ya bajeti na maelezo kuhusu hali ya uchumi kwa ujumla.

Alisema mara baada ya Bunge kukamilisha kazi ya kujadili na kupitisha makadirio ya matumizi ya wizara zote, muswada wa fedha za matumizi utawasilishwa bungeni na kupitishwa mfululizo katika hatua zote kwa mujibu wa kanuni namba 105.

Alisema muswada huo hautajadiliwa bungeni kama ilivyo miswada mingine, utasomwa na kupitishwa moja kwa moja maana unahitimisha mjadala wa jumla kwa kutaja jumla ya fedha zote za matumizi ya serikali zilizopitishwa na Bunge kwa mwaka huo wa fedha.

Kiu kubwa ya baadhi ya watu ni kuona hatua zipi zimechukuliwa na serikali dhidi ya watu waliotakiwa kuwajibishwa baada ya kamati teule ya Bunge iliyokuwa ikiongozwa na Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, kubaini ukiukwaji wa sheria ya manunuzi ya umma, ambako kulifanya Kampuni ya Richmond kupewa zabuni ya kuzalisha umeme.

Ripoti ya kamati teule iliwasilishwa katika mkutano wa 10 wa Bunge na tangu wakati huo serikali imekuwa ikitoa sababu kadhaa za kutokamilisha utekelezaji wa maazimio hayo, kwa madai kuwa mambo mengine yalihitaji kuangalia sheria zaidi, huku mengine yakihitaji kufika kwa rais ili yatolewe uamuzi.

Wakati baadhi ya watuhumiwa wakiendelea kuwajibika katika ofisi za umma, mmoja wa watuhumiwa hao, Gray Mgonja, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, amefikishwa mahakamani akikabiliwa na makosa 10 ya kutumia vibaya madaraka yake, kwa kutoa msamaha kwa Kampuni ya Alex Stewart ambayo iliisababishia serikali hasara ya sh bilioni 11.

TANZANIA,TANZANIA,OH TANZANIA!!


Naomba nikuulize swali; Kwenye muziki unapenda zaidi ujumbe uliomo au midundo kwa maana ya beats? Kwako wewe muziki ni nini? Usiharakishe kunijibu. Fikiri kwanza.

Wakati unafikiri ngoja nikupe jibu langu.Mara nyingi huwa napenda wimbo wenye ujumbe. Midundo ikiwa imetulia huwa nazama pia.Ndio maana nampenda sana Oliver Mutukudzi(mwanamuziki kutoka Zimbabwe) wakati mara nyingi sielewi anachokiongelea mpaka pale ninapopewa tafsiri. Napenda jinsi anavyocharaza gitaa lake na kutawala jukwaa. Napenda muziki kwa sababu naamini muziki ni universal language(lugha ya dunia).

Miongoni mwa nyimbo ambazo nimezisikia hivi karibuni na kupenda ujumbe na midundo ni kutoka kwa mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania anayekwenda kwa jina Roma(pichani). Jina la wimbo wake ni Tanzania. Msikilize Roma kwa kubonyeza player hapo chini kisha uniambie kama ujumbe uliomo kwenye wimbo huu unakugusa au la.

Tuesday, May 19, 2009

Malecela: Busanda CCM maji shingoni

• Awaangukia wafanyabiashara kuiokoa


na Kulwa Karedia, Busanda




MAKAMU Mwenyekiti mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, John Malecela, maarufu Tingatinga, amekiri kuwa chama hicho kinakabiliwa na upinzani mkali katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Busanda na kwamba sasa maji yako shingoni.

Akizungumza na wafanyabiashara zaidi ya 50 katika soko kuu la mji mdogo wa Katoro, jana, ikiwa ni mwendelezo wa kampeni za ubunge katika Jimbo la Busanda, Malecela alisema hali ya mambo si shwari na kuwaomba kuiunga mkono CCM.

“Nimewatembelea hapa kujua matatizo yenu pamoja na kuwaambia kwamba, tunakabiliwa na uchaguzi ndani ya jimbo hili, nawaomba mtumie fursa hii kuchagua CCM ili iweze kumaliza matatizo madogo madogo yaliyopo,” alisema.

Malecela ambaye alifika sokoni hapo majira ya saa 7 mchana akiwa na gari aina ya Toyota Land Cruiser, yenye namba za usajili T 509 AFZ, aliwataka wafanyabiashara kutobabaishwa na sera za vyama vingine.

Kauli ya Malecela ilionekana kuwa mwiba mchungu kwa wafanyabiashara hao ambao waligeuka na kumweleza kuwa umefika wakati wa kufanya mabadiliko.

“Tunasema kama CCM mnasema maji yamefika shingoni, tunasema ni haki yenu kwani sisi tukiingia humo tutazama, sasa kwanini tujitafutie matatizo hivyo,” alisema mmoja wa wafanyabiashara hao, Marando Mayalla.

Alisema kwa kipindi kirefu CCM imetumia mwanya wa kuwadanganya katika masuala mbalimbali ya kijamii, ikiwamo ahadi ya kupelekewa umeme, lakini imeshindwa kutimiza.

“Tumekuwa watu wa kudanganywa kila mwaka sisi… tumeahidiwa umeme hapa miaka mingi, leo tena mnakuja na sera eti ya kuwachagua, tunasema kila jambo lina mwanzo na mwisho wake,” alisema Mayalla kwa niaba ya wenzake.

Alisema hata kitendo cha CCM kumrejesha mmoja wa wanasiasa maarufu wa chama hicho, aliyegoma kupanda jukwaani, Donald Maxi, hakutasaidia kitu kwani mwenyewe amejimaliza kisiasa.

“Sisi tunasema hata huyo Maxi ambaye mmeamua kumrudisha CCM kwa ajili ya kusaidia kampeni, amechemsha kwani huko ni kujimaliza kisiasa... inakuwaje agome kupanda jukwaani mpaka rais aaingilie kati?” alihoji Mayalla.

Kutokana na kauli za wafanyabiashara hao, Malecela aliamua kuondoka eneo hilo, huku akinyonyeshewa vidole kwa alama ya V ambayo hutumiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika kupeana salamu za chama.

Tangu CCM ilipozindua kampeni zake, imekuwa na wakati mgumu kutokana na viongozi wake kuzomewa karibu mikutano yote inayofanywa hali ambayo imesababisha mgawanyiko mkubwa ndani ya chama hicho.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe anatarajiwa kuwasili leo jimboni hapa na kuanza kutumia helikopita kumnadi mgombea wa chama hicho, Finias Magessa.

Ratiba inaonyesha kuwa, Mbowe anatarajiwa kufanya mikutano saba kwa siku moja ambapo ataanzia katika viijiji vya Rwamgasa, Kaseme, Katoro na Ibondo kwa nyakati tofauti.

Katika hatua nyingine, vijana wa CCM, maarufu kama Green Guard, jana waligeuza Kijiji cha Nyachilulula kuwa uwanja wa vujo baada ya kutembeza kipigo kwa baadhi ya wafuasi wa CHADEMA.

Tukio hilo ambalo limeonekana wazi kubadili sura ya kampeni, lilitokea majira ya saa 5:40 asubuhi kijijini hapo wakati CCM ilipokuwa ikimnadi mgombea wake, Lolencia Bukwimba, ambaye amekuwa na wakati mgumu kutokana na kuzomewa kila anapopanda jukwaani.

Tangu CCM walipofanya mkutano wao katika Kijiji cha Katoro wiki iliyopita, wamekuwa wakitumia vijana wa Green Guard kukamata na kuwapiga vijana wanaosadikiwa kuwa wafuasi wa vyama vya upinzani, jambo ambalo limezua malalamiko mengi.

Wakati mkutano huo wa Nyachilulula ukiwa unaendelea, vijana watatu ambao wanasaidikiwa kuwa ni wafuasi wa CHADEMA, walipita karibu na eneo la mkutano, huku wakipeperusha bendera ya chama hicho.

Vijana hao wakiendelea na safari, walishitukia wakifuatwa na gari aina ya Toyota Prado, yenye namba za usajili T 718 na waliokuwamo ndani kushuka ghafla na kuanza kuwapiga.

Waliopigwa ni pamoja na Chacha Magabe na Lucas Tigamanya ambao baada ya kipigo hicho haikujulikana mara moja walipelekwa wapi.

Wakati tukio hilo linaendelea, Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango, alikuwa jukwaani akimnadi mgombea wa CCM.

Hata hivyo, lawama nyingi zimeelekezwa kwa Jeshi la Polisi kwani hawahudhurii mikutano mingi ya kampeni.

Mmoja wa wanakijiji wa Nyachilulula, Mabula Shijja alisema amesikitishwa na kitendo cha CCM kupiga watu kila wanapofanya mikutano.

“Hii ni tabia mbaya kwani CCM sasa wamekuwa na tabia ya kupiga watu kila wanapofanya mkutano, juzi tumeshuhudia pale Katoro watu walivyopigwa vibaya na kuswekwa ndani,” alisema Shijja.

Alisema umefika wakati hatua za haraka zichukuliwe ili kudhibiti hali hiyo ambayo inavunja misingi ya demokrasia.

Akimnadi mgombea wake, Kilango aliwataka wakazi wa Kijiji cha Nyachilulula, kutumia fursa ya kuchagua kiongozi bila ya shinikizo lolote la kisiasa.

“Tumieni fursa yenu kuhakikisha kwamba mnachagua kiongozi ambaye mnamtaka, msibabaishwe na vita ya mafisadi inayoendelea ndani ya chama chetu.

“Ni ukweli usiopingika kwamba ndani ya chama changu kuna baadhi ya wananchama na viongozi wanaojihusisha na ufisadi, lakini si wote,” alisema Kilango.

Katika hatua nyingine, askari polisi zaidi ya 45 ambao wamepelekwa jimboni Busanda kwa ajili ya shughuli za ulinzi, wamelalamikia posho ya sh 1,000 ambayo wanalipwa kwa siku.

Wakizungunza jana mjini hapa, na kuomba majina yao yasitajwe gazetini, askari hao walisema kiasi hicho ni kidogo ambacho hakiwezi kukidhi mahitaji yao ya kila siku.

“Hata wewe fikiria kwamba tumeacha familia zetu, ndugu yangu tunalipwa sh 1,000 kwa siku, unadhani inaingia akilini? Basi ndiyo hivyo tena, hatuwezi kulalamika kwa wakubwa,” alisema mmoja wa askari hao.

Tuesday, April 28, 2009

TUGAWANE UMASIKINI” MAANA YAKE NINI?


Juma Nature ni miongoni mwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya ambao huathiri jamii moja kwa moja kila watoapo albamu au wimbo.Matumizi yake ya lugha,mtindo wake wa kughani au kurap,uhalisia wa kitu anachokiongelea nk ni miongoni mwa mambo ambayo yanamfanya atambe na akubalike zaidi.


Hivi karibuni alitoa albamu ambayo ameipa jina la “Tugawane Umasikini”. Baada ya hapo kumekuwa na tafsiri mbalimbali kuhusu “kugawana umasikini”.Bila shaka umeshasikia mtu akikuambia ah…leo ni weekend bwana…ngoja tukagawane umasikini.Starehe mbalimbali zikiwemo ngono,pombe nk zimekuwa ni “kugawana umasikini”.


Lakini yeye mwenyewe alikusudia au kumaanisha nini alipozungumzia “Kugawana Umasikini”? Ili kupata jibu kamili nilimtafuta Nature na kufanya naye mahojiano yafuatayo;


MK:Mambo vipi Nature?Umeshamaliza tour ya kuzindua albamu yako?


JN: Mambo poa kabisa ndugu yangu.Tour naweza kusema bado inaendelea ingawa baada ya kutembelea mikoa kadhaa hivi sasa nimerejea nyumbani Dar kwa ajili ya mapumziko kidogo na kuangalia masuala ya familia.


MK: Nimekutafuta kwa ajili ya kutaka kujua kitu kimoja; hivi karibuni umetoa albamu ambayo umeiita Tugawane Umasikini. Baada ya kutoka kwa albamu hiyo kumekuwepo na tafsiri mbalimbali kuhusu “kugawana umasikini”.Wengine wanasema kugawana umasikini ni pamoja na kugida maji kwa sana,ngono(zikiwemo zembe) na kwa ujumla kuamua tu kuishi bila kufanya kazi kwa juhudi kwa sababu tayari wengi wetu tu masikini na hivyo hakuna la kufanya.Je, wewe ulimaanisha nini haswa ulipotaka kuzungumzia “kugawana umasikini”?


JN: Ahahahaha, labda hapo naweza kusema hiyo ni kazi nzima ya fasihi kwamba kila mtu anaweza kuupokea ujumbe atakavyo au apendavyo na wote wakawa sahihi! Kimsingi nilichomaanisha ni kwamba kutokana na ukweli kwamba nchi yetu na wengi wa wanachi wake bado ni masikini, ni jambo muhimu sana kusaidiana.


Pamoja na umasikini tulionao,endapo tutaamua kugawana hicho hicho kidogo tulichonacho basi kwa pamoja tutaweza kuinuana.Baba wa Taifa,Mwalimu Nyerere alipenda sana kutukumbusha kuhusu “Umoja ni Nguvu”.Hapo ndipo alipoongelea sana habari za Ujamaa na Kujitegemea.Leo hii tumesahau misingi ile na ndio maana labda tunaendelea kuwa masikini.Lakini mimi nikiwa nacho kidogo na nikamsaidia mwenzangu,basi kesho si ajabu na yeye akainuka na kumsaidia yule ama yule.Kwa mwendo huo tutafika mahali pazuri zaidi.Isitoshe hatuwezi kuzungumzia utajiri wakati sisi ni masikini.


Hivyo ndivyo nilivyoomanisha na ndivyo nilivyokusudia.Wanaopotosha au kujaribu kupindisha maana halisi wanafanya hivyo kwa sababu zao wenyewe zikiwemo kujifariji nk. Lakini kama nilivyotangulia kusema hapo juu,hiyo ni kazi ya fasihi na hivyo siwezi kuwatolea macho au kuwalaumu. (more…)

Muungano waibua malumbano makali katika televisheni ya taifa

Na Salim Said

MVUTANO mkali umeibuka miongoni mwa wasomi, wanasiasa na serikali katika mjadala kuhusu kero za Muungano uliofanyika jijini Dar es Salaam juzi.


Katika mjadala huo, baadhi ya washiriki walikua wakinyoosheana vidole na kutuhumiana kuwa, ndio wanaosababisha kukua na usugu wa kero za Muungano wa Tangayika na Zanzibar.


Mjadala huo ambao ulirushwa na Kituo cha Televesheni TBC1 uliwashirikisha baadhi ya wasomi, viongozi wa serikali na wanasiasa..


Waziri wa Nchi katika ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Muhmmad Seif Khatib alisema muungano umeimarika na kwamba ndoto za waasisi wake, ambao ni mwalimu Julius Nyerere na hayati Abeid Aman Karume zimetimia.


Kauli hiyo pia, iliungwa mkono na Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Azaveli Lwaitama ambaye alisema muungano umeimarika na kwamba, falsafa ya waasisi imetimia.


“Hata ukimuuliza ndugu yangu Duni hapo, atakwambia yeye ni Mtanzania, kero zinakuzwa na wanasiasa ambao hawajaelewa, yaliyokuwamo katika vichwa vya waasisi wa muungano huu” alisema Dk Lwaitama


Kauli hizo zilionyesha kumkera Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Juma Duni Haji ambaye katika kujibu hoja hiyo alisema, “kama kuimarika kwa muungano ni kuwepo kwa kero nyingi na matatizo, basi umeimarika lakini kama ni utatuzi wa matatizo na kero hizo, basi bado haujaimarika”.


“Katika mambo ambayo siyapendi na yananikera sana ni kuufananisha muungano huu kuwa ni wa mke na mume au mkubwa na mdogo. Huu ni muungano wa nchi mbili. Mimi nikiwa Katibu wa Wizara ya Fedha tuliisaidia serikali ya muungano dola 15 milioni za Marekani kulipa deni la Benki ya Dunia,” alisisitiza Duni.


Jambo hilo, lilimfanya muongoza mjadala huo ambaye ni mtangazaji wa TBC1, kumuomba radhi mwanasiasa huyo na kuruhusu mjadala huo kuendelea.


Duni aliendelea kutoa mifano ya kutoimarika kwa muungano huo kuwa, ni pamoja na kufukuzwa katika chama, kwa Rais mstaafu, Aboud Jumbe na maalim Seif Sharif Hamad, ambaye alikuwa waziri kiongozi wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kutoka na kesi za muungano.


“Muungano lazima ulete faida kwa wananchi kisiasa, kiusalama na kiuchumi lakini Wazanzibari wanahoji kuhusu fedha za misaada na mikopo zinazoingia nchini kwa jina la Tanzania, kwa nini hawapati,” alihoji Duni


Alisema, jambo muhimu ni kushughulikia kero za muungano na si kuwa, mtu akisema aitwe katika vikao vya kamati kuu ya chama na kunyamazishwa au kuadhibiwa.


Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari, Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (Misa- Tan), Ayoub Rioba alisema, kama kuna mawasiliano yanayoeleweka, baina ya viongozi na wananchi, matatizo ya kero za muungano yatamalizika.


“Kama tutakuwa na mawasiliano imara baina ya pande mbili hizi, tatizo ni dogo sana lakini pia tuthamini michango ya mijadala kama hii, kwa kuwa bado sisi tunayo fursa ya kujadiliana, wenzetu wanatafuta lakini hawapati fursa ya kujadiliana” alisena Rioba.


Katika hilo, Dk Lwaitama alisistiza kuwa, dhamira ya waasisi ilikuwa ni umoja na mshikamano wa Watanzania na Waafrika lakini matatizo na kero ni jambo la kawaida.


Kwa upande wake waziri Khatibu alisisitiza kuwa, uhuru, usalama, amani na uchumi wa Zanzibar unategemea serikali ya muungano iliyopatikana baada ya kuungana kwa Zanzibar na Tanganyika mwaka 1964.


“Muungano ni wa binadamu wala si wa malaika, matatizo hayaepukiki lakini tunafanya jitihada mbalimbali za kutatua kero na matatizo hayo” alisema Khatib.

Serikali yamgeuka Reginald Mengi kwa kauli ya mapapa wa ufisadi


Ramadhan Semtawa na Leon Bahati


MAWAZIRI wawili, Sophia Simba na George Mkuchika jana walimshambulia mfanyabiashara maarufu nchini, Reginald Mengi ambaye wiki iliyopita alitangaza majina ya wafanyabiashara watano wenye asili ya Kiasia, akisema ni mafisadi waliokubuhu.


Simba, ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) na Mkuchika, Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo walisema mfanyabiashara huyo wa jijini Dar es salaam "amechemsha".


Mengi alitangaza majina ya wafanyabiashara hao Alhamisi iliyopita akisema ni kati ya watu wasiozidi 10 ambao alidai wanaifilisi nchi na kutaka wadhibitiwe mapema kabla hawajaitingisha na kuiyumbisha nchi.


Hata hivyo, Mengi, ambaye alidai katika taarifa yake kuwa juhudi za Rais Jakaya Kikwete zinakwamishwa na watu hao, hakueleza jinsi watano hao wanavyoitafuna nchi zaidi ya kusema kuwa wanatorosha fedha wanazozipata 'kifisadi'.


Jana, kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam mawaziri hao wawili walitoa kauli za kumshambulia mwenyekiti huyo mtendaji wa makampuni ya IPP, kauli ambazo zinadokeza mtazamo wa serikali katika mjadala unaoendelea wa vita dhidi ya ufisadi na vinara wake.


Waziri Simba, ambaye wizara yake pia inawajibika katika vita dhidi ya ufisadi, alisema: "Kakosea... watoto wa mjini wanasema kachemsha."


Simba alitoa msimamo huo jijini Dar es Salaam jana muda mfupi baada ya kufungua semina ya wadau wa vyama vya siasa kuhusu namna ya kuiboresha Sheria ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995.


Simba alisema Mengi hana mamlaka hayo ya kutaja watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi.


Kabla ya kujibu swali kuhusu kitendo cha Mengi, ambaye anamiliki televisheni ya ITV na kituo cha redio cha Radio One Stereo, kutaja majina ya watu hao aliowaita mafisadi papa, Simba alihoji: " Hapa kuna mtu wa ITV?."


Baadaye alisema: "Sikilizeni, kwanza kitendo alichokifanya Mengi si sahihi, kakosea hawezi kuhukumu watu, mamlaka hayo anatoa wapi?"


Simba, huku akionekana kama mtu ambaye alikuwa akitafuta jukwaa kuzungumzia suala hilo, alisema Mengi amekosea kwa kuwa baadhi ya watu aliowataja wana kesi mahakamani.


"Anahukumu watu," alisema. "Kuna mtu kama Jeetu (Patel) ana kesi mahakamani (EPA), sasa unapokuja kusema ni fisadi wakati mahakama haijathibitisha, unakuwa na maana gani.


"Kwanza kwanini awatuhumu wafanyabiashara wenzake tu, ina maana si ana nia mbaya nao."


Alisema Mengi amechukua uamuzi huo kama vile serikali, wakati serikali ipo siku zote na imekuwa ikifanya kazi zake kwa umakini kwa kufuata misingi ya sheria.


"Serikali ipo na inafanya kazi kwa misingi ya sheria, sasa yeye kukaa na kutangaza watu nasema si sahihi kabisa. Mahakama pekee ndiyo inaweza kumtia mtu hatiani, lakini huwezi kuhukumu watu kama hakuna mamlaka."


Waziri Simba, ambaye pia ni mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), alisema Mengi hapaswi kutumia vyombo vyake vibaya.


"Asitumie vyombo vyake kufanya atakavyo yeye. Huwezi kukaa katika chombo chako na kuanza kuhukumu watu. Kila mtu akifanya hivyo itakuaje," alihoji.


Akiongea na Mwananchi baada ya kupata taarifa za kauli ya Simba, Mengi alisema: "Namuombea kwa Mwenyezi Mungu na kwa maskini wa Tanzania ili wamsamehe kwa sababu hajui anenalo."


Mengi hakutaka kuzungumza zaidi kuhusu hatua hiyo ya Mama Simba.


Naye Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika aliwaambia waandishi wa habari kuwa serikali itamchukulia hatua za kisheria Mengi iwapo itabainika alikiuka taratibu na kanuni za nchi kwa kutangaza majina ya watu anaowatuhumu kwa ufisadi.


Mkuchika alisema jijini Dar es Salaam jana kwa sasa serikali inafanya uchunguzi juu ya suala hilo na itatumia mikanda ya video pamoja na maelezo ya kimaandishi aliyoyatoa Mengi siku alipokutana na waandishi wa habari.


"Tumekusudia kupata ule mkanda wa video, pia tusome maelezo yake ya kimaandishi... tukigundua kuna mahala ambapo sheria haikuzingatiwa, (Mengi) atachukuliwa hatua," alisema Mkuchika.


Mkuchika alisema serikali imepokea malalamiko mengi kutoka kwa watu wengi, wakishutumu hatua iliyochukuliwa na Mengi, ambaye pia anamiliki viwanda vya vinywaji.


Bila kutaka kuwataja majina, Mkuchika alisema miongoni mwa walalamikaji, wapo walioeleza kuwa vyombo vya habari vya mfanyabiashara huyo havikuwatendea haki watuhumiwa waliotajwa kuwa ni mafisadi wakuu.


Alisema ni kutokana na vyombo hivyo kuwataja majina watuhumiwa bila ya kuwapa fursa ya kujibu madai dhidi yao.


Waziri Mkuchika alipotakiwa kueleza siku ambayo uchunguzi huo utakamilika, alijibu wananchi wanapaswa kuwa watulivu kwa sababu serikali ikimaliza kuchunguza, itawatangazia yale waliyobaini.


Hii ni mara ya pili katika kipindi cha miezi takribani mitatu kwa Mengi kuingia katika mvutano na serikali baada ya kuvutana mapema mwaka huu na Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha kutokana na kutangaza kuwa kuna mipango ya kumfilisi na kumuua.


Mengi pia amewahi kujikuta katika malumbano na watendaji wa serikali hasa na waziri wa zamani wa nchi, ofisi ya rais (utawala bora), Wilson Masilingi alipotoa tuhuma kuwa suala la utoaji zabuni ya ununuzi wa hoteli ya Kilimanjaro, hivi sasa inajulikana kama Kilimanjaro Kempiski, kulikuwa na kitu alichokiita "mchezo mchafu".


Suala hilo liliamsha malumbano makali, lakini liliishia hewani.


Katika tuhuma za wiki iliyopita, Mengi aliwahusisha wafanyabiashara hao watano na kashfa za wizi wa fedha kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), utoaji zabuni ya ufuaji umeme wa dharura kwa kampuni ya Richmond Development (LLC) na uuzwaji wa jengo la Mfuko wa Hifadhi ya Taifa ya Jamii (NSSF).


Mengi, ambaye kituo chake cha televisheni cha ITV kiliwahi kuendesha mchezo mkubwa wa bahati nasibu ya Jackpot Bingo, pia aliitaja Bahati Nasibu kuwa katika tuhuma hizo, pamoja na mradi wa makaa ya mawe wa Mchuchuma.

Monday, April 27, 2009

Simba SC uuuh!


Timu soka ya Simba ya Dar es Salaam jana ilijihakikishia kucheza michuano ya kimataifa mwakani, baada ya kuifunga Polisi Dodoma mabao 2-0 katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini hapa.

Matokeo hayo yamewafanya mashabiki wa Simba kupumua, kutokana na kutokuwa na raha kwa kukosa michuano ya kimataifa inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa mwaka huu, hivyo jana walikuwa wakisubiri kwa hamu kubwa matokeo ya mchezo huo. Simba iliyoingia uwanjani ikiwa na pointi 37 ilikuwa ikihitaji ushindi ili ijihakikishie 'kupanda ndege' mwakani katika michuano ya kimataifa, ambapo kinyume na matokeo hayo ingejiweka pabaya, kwani Mtibwa Sugar iliyokuwa na pointi 35 nayo jana ilicheza na Polisi Morogoro na kushinda mabao 3-2.

Simba sasa imefikisha pointi 40, wakati Mtibwa ina pointi 38. Mabao ya Simba yalifungwa na Haruna Moshi dakika ya 69, kisha Mohammed Kijuso alifunga bao la pili dakika ya 81, Beki Said Gabeza alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 72 kutokana na mchezo mbaya. Kutoka Mbeya, Merali Chawe anaripoti kuwa Moro United jana iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya. Moro United ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya tisa mfungaji akiwa Thomas Mourice baada ya kupokea pasi ya Amri Kiemba.

Prisons ilisawazisha bao hilo dakika ya 40 mfungaji akiwa Fred Chudu, baada ya kipa Haji Macharazi wa Moro kuutema mpira na kumkuta mfungaji. Moro United ilipata bao la pili dakika ya 68, baada ya beki David Mwantike kujifunga kwa kichwa katika harakati za kuokoa, ambapo matokeo hayo yameifanya Moro United ifikishe pointi 25. Matokeo hayo yanaipa nafasi Moro United kubaki katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao, badala yake Polisi Moro inashuka daraja kutokana na kufungwa mabao 3-2 na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Timu zote hizo zina pointi 25, ambapo ukiangalia uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa zote ni 0-0, ambapo Moro United imefunga mabao 31 na imefungwa 31, wakati Polisi Moro imefunga mabao 25 na imefungwa 25. Kulingana na kanuni za ligi hiyo zilizotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kama timu zitafungana pointi itatazamwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa, lakini pia kama zitafungana itaangaliwa timu yenye mabao mengi ya kufunga, ambapo kwa timu hizo mbili ni Moro United yenye mabao 31 ukilinganisha na 25 ya Polisi.

"Ikiwa timu mbili zitalingana kwa pointi baada ya michezo mshindi atapatikana kwa tofauti bora ya magoli ya kufungwa na kufunga, kama tofauti hiyo haitoi mshindi, mshindi atakuwa ni mwenye magoli mengi ya kufunga, kama pia magoli ya kufunga hayatoi mshindi, basi mshindi atakuwa ni yule atakayekuwa na pointi nyingi kwenye michezo miwili iliyohusisha timu hizi mbili.

“Na kama pia michezo hiyo haitoi mshindi, mshindi atakuwa yule aliyefunga magoli mengi zaidi katika mchezo wa ugenini uliozihusisha timu hizi mbili, iwapo bado haitoi mshindi, mshindi atakuwa aliyefunga magoli mengi ya ugenini katika msimu mzima, iwapo bado haitoi mshindi timu hizi zitacheza mchezo mmoja katika uwanja utakaochaguliwa na TFF, na taratibu zote za kupata mshindi zitafuatwa kama mchezo wa fainali, " inasema kanuni ya sita ya ligi kuhusiana na mshindi.

Kwa mujibu wa Mwandishi John Nditi, mabao ya Mtibwa yalifungwa na Said Mkopi dakika ya pili, kabla ya Ally Moshi kusawazisha dakika ya tatu, kisha Soud Abdallah wa Mtibwa kufunga la pili dakika ya 16, Polisi ikasawazisha dakika ya 17 mfungaji akiwa Fred Hagai. Bao la ushindi la Mtibwa lilifungwa dakika ya 44 na Shaaban Nditi. Kutoka Mwanza, Toto African iliifunga Azam FC bao 1-0, lililofungwa dakika ya 51 na Hussein Sued, matokeo ambayo yameifanya Toto ifikishe pointi 28 hivyo kuepuka kushuka daraja.

Naye Mwandishi Wetu anaripoti kuwa mchezo kati ya Yanga na Villa Squad uliokuwa ufanyike jana ulikwama kutokana na mvua kubwa iliyonyesha, hivyo Uwanja wa Uhuru kujaa maji. Kutokana na michezo hiyo ya mwisho ya ligi jana, Polisi Moro sasa inaungana na Polisi Dodoma yenye pointi 18 na Villa Squad yenye pointi 15 kushuka daraja, ambapo mwakani zitacheza ligi daraja la kwanza.Yanga ndiyo bingwa wa ligi hiyo, wakati Simba imeshika nafasi ya pili.

Friday, April 17, 2009

Fuvu la binadamu wa kale!


Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) fuvu la binadamu wa kale, Zinjathropus, wakati wa mkutano kuhusu maadhimisho ya miaka 50 ya ugunduzi wa fuvu hilo, Dar es Salaam jana.

Ngassa ngoma nzito ughaibuni


Winga wa Yanga ya Dar es Salaam na timu ya soka ya taifa 'Taifa Stars', Mrisho Ngassa ameanza majaribio katika timu ya West Ham United ya nchini Uingereza, lakini kukiwa na wachezaji wengi wanaowania pia kusajiliwa na timu hiyo.

Akizungumza na gazeti hili kwa simu jana, Mohammed Sadick, ambaye ni Mtanzania anayeishi nchini humo, alisema pamoja na kuwa na matumaini huenda Ngassa akafanikiwa, lakini kazi ya ziada itabidi aifanye ili kuipata nafasi hiyo. "Niliposikia kuwa Ngassa anakuja huku, nilifuatilia mambo mbalimbali ndani ya timu anayokuja, nikagundua anatakiwa aongeze juhudi za ziada uwanjani ili kuwashawishi wamchukue.

"Namfahamu Ngassa ana uwezo mkubwa, kinachotakiwa apambane, maana vijana wanaotakiwa ni wachache, wakati wao wapo wengi, huku wengine wakitoka nchi zenye majina makubwa kisoka Afrika na hata hapa Uingereza," alisema Sadick. Hata hivyo alisema katika siku mbili za mazoezi, ameonyesha mwelekeo, ingawa idadi kubwa ya wachezaji waliopo katika majaribio ambao wanazidi 20, huku wakitakiwa watatu inamtisha.

Naye mchezaji mmoja wa Yanga, ambaye ni rafiki wa karibu wa Ngassa, alilieleza gazeti hili jana kuwa amezungumza na mchezaji huyo juzi na kumwambia ameanza vizuri, lakini idadi ya wanaotakiwa inamwogopesha. "Amenambia wapo wachezaji 20 wengine wanatoka Nigeria, Senegal, Afrika Kusini na sehemu nyingine, lakini wanatakiwa watatu, sasa nimemweleza asife moyo ndio mapambano yenyewe hayo, aongeze juhudi uwanjani.

"Amenielewa, tunamtakia heri, huku pia wadau wengine naamini nao wanamtakia mafanikio mazuri, hakuna kisichowezekana chini ya jua, " alisema mchezaji huyo. Ngassa ambaye ni mtoto wa kiungo wa zamani wa Pamba, Simba na timu ya taifa 'Taifa Stars', Khalfan Ngassa 'Babu', aliondoka Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki kwenda nchini Uingereza kufanya majaribio ya kucheza soka katika kikosi cha vijana cha timu ya West Ham ya huko inayoshiriki Ligi Kuu ya England.

Kikwete awajia juu mawaziri watukanao

Imeandikwa na Maulid Ahmed, Saudi Arabia; Tarehe: 17th April 2009 @ 10:34

Rais Jakaya Kikwete ameelezea kukerwa na vitendo vya baadhi ya mawaziri wa nchi za Afrika Mashariki kutumia lugha za matusi na kuikejeli Tanzania kutokana na msimamo wake wa kutokubali suala la ardhi na ajira liwe la Afrika Mashariki kwa sasa. Rais Kikwete alielezea masikitiko yake hayo juzi wakati akijibu maswali ya Watanzania waishio hapa wakati alipokutana nao katika Hoteli ya Riyadh Palace.

Ingawa Rais Kikwete hakutaja mawaziri hao ni wa nchi gani, lakini hivi karibuni zimekuwapo taarifa kuwa baadhi ya mawaziri wa Kenya wamekuwa wakiikejeli na kupingana na Tanzania kwa msimamo wake wa kutaka suala la ugawaji ardhi kwa wananchi wa Afrika Mashariki lisiingizwe kwenye masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, bali nchi husika iwe na mamlaka juu ya umilikishwaji huo wa ardhi. Rais Kikwete alisema: “kinachonisumbua sasa juu ya suala hili ni jinsi linavyojadiliwa kwa kejeli, waziri tu anatukana nchi nyingine, lugha zinazotumiwa hazitasaidia kujenga Afrika Mashariki, silifurahii hili la kutukana nchi nyingine.

“Kama hili la ardhi sasa haliwezekani tusigeuze kuwa kama hilo haliwezekani basi Jumuiya ya Afrika Mashariki haiwezekani, kama kwa sasa suala la ardhi ni gumu liachwe yafanywe mengine yanayowezekana na wakati ukifika litajadiliwa”. Mbali na hilo, Rais Kikwete ambaye alimaliza ziara yake jana, aliwambia Watanzania hao kuwa kutokana na hali ya mvua mwaka huu kutokuwa nzuri nchini, kutakuwa na upungufu wa chakula.

Alisema uhaba wa mvua upo katika mikoa ya Pwani, Tanga, Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Morogoro na kuongeza: “Lakini tutajitahidi kukabiliana na uhaba huo”. Aliwaasa Watanzania hao kukumbuka nyumbani kwa kupeleka maendeleo na kuwasaidia ndugu zao na si kujisahau na wanaporejea nyumbani wanajikuta wakiwa na maisha magumu. Aliwataka waishi hapa kwa kuzingatia sheria za nchi na kuongeza: “Huwezi kuishi hapa kwa sheria zako, watakushughulikia, ukifanya makusudi kuvunja sheria hutatunyima usingizi, lakini ukionewa ubalozi utakusaidia”.

Akijibu swali la Mtanzania aliyetaka kuanzishwe shule ya Afrika Mashariki ili watoto wasome kwa kufuata mtaala wa Afrika Mashariki, Rais Kikwete aliwataka mabalozi wa nchi za Afrika Mashariki kukaa na kuanzisha shule hiyo na serikali zao zitasaidia kupeleka mitaala ya kufundishia. Kuhusu uraia wa nchi mbili, alisema Watanzania wengi waishio nje wanalitaka hilo, na kwa sasa suala linafanyiwa kazi.

Katika hatua nyingine, mke wa Rais, Salma Kikwete, aliwambia wanawake Watanzania wanaoishi hapa, kuwafundisha watoto wao utamaduni wa Kitanzania na lugha ya Kiswahili. “Asiyekuwa na utamaduni ni mtumwa, wafundisheni watoto utamaduni wa nyumbani na nyinyi kumbukeni kusaidia nyumbani,” aliwambia. Wakati huohuo, Rais amesema kuanzia sasa Tanzania itaanza kupata mikopo yenye masharti nafuu kutoka taasisi za fedha duniani kutokana na utendaji wake kuwa mzuri.

Tanzania ni miongoni mwa nchi tano za Afrika zilizofanya vizuri kiutendaji ambapo Rais Kikwete alisema: "Kutokana na utendaji wetu mzuri mlango wa kupata mikopo sasa utafunguliwa na tutafanya maendeleo zaidi." Akifanya majumuisho ya ziara yake mjini hapa, Rais aliwataka wafanyabiashara wa Tanzania kujitayarisha kuchangamkia uwekezaji kutoka Saudi Arabia.

"Tujitayarishe katika maeneo ambayo wafanyabiashara wa Saudi Arabia wameonyesha nia, mfano katika kilimo, ili wakija wakute watu wako tayari kushirikiana nao… wamesema wana dola trilioni 1.6 na kati ya hizo dola bilioni 60 wamezitenga kwa utalii nasi tutumie nafasi hiyo," alisema. Akijibu swali aliloulizwa sababu za utawala wake kupata misaada mingi kuliko mikopo, alisema: "Kila kitu kina wakati wake na kukaa kwangu miaka 10 nikiwa Waziri wa Mambo ya Nje, kumenisaidia kupata marafiki wengi ambao sasa wananisaidia kupata misaada katika nchi zao kama Marekani, Uingereza, Japan na Ufaransa".

Alisema licha ya Tanzania kupata misaada kutoka Saudi Arabia kama kusaidia ujenzi wa daraja la Mkapa lakini bado haijatumia sawasawa fursa za kupata misaada hiyo na kuongeza kuwa sasa itaitumia nafasi hiyo. Alisema ziara hiyo ya kikazi ya siku tatu imekuwa na mafanikio na sasa Tanzania ina matumaini ya kuuza bidhaa zake Saudi Arabia.

DECI sasa kizaazaa

• Watangaza kufunga ofisi zao nchi nzima


na Ratifa Baranyikwa na Lucy Ngowi




SIKU moja baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutangaza msimamo wa serikali wa kutounga mkono shughuli zinazofanywa na Kampuni ya Development of Entrepreneurship for Community Initiative (DECI), viongozi waasisi wa kampuni hiyo wamejitokeza hadharani na kupinga msimamo huo wa serikali.

Mbali ya kutangaza msimamo huo, DECI imetangaza kufunga ofisi za matawi yake yote 36 nchi nzima ili kupisha majadiliano yanayoendelea kati yake na serikali.

Waaasisi hao wa DECI ambao walijitokeza kwa mara ya kwanza jana na kujitambulisha kwa majina na vyeo vyao, walikanusha vikali kauli ya Waziri Mkuu Pinda aliyeuelezea mchezo wao kuwa ni upatu na ujanja ujanja wenye mwisho mbaya.

Wakizungumza kwa kupokezana, waasisi hao, Timoth Ole Loeiting’ye, Meneja Ufundi na Ushauri, Arbogast Kipilimba na Mwenyekiti wa Bodi, Jackson Mtaresi, walirejea hoja waliyopata kuieleza siku zilizopita kwamba, DECI ni matokeo ya maono na ufunuo walioupata kutoka kwa Mungu kwa njia ya sala kabla ya kuianzisha.

Waasisi hao ambao walikuwa wakizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam, jana, waliwahimiza washiriki wa mchezo huo kuendelea kupanda na kuvuna, wakisisitiza kuwa, kampuni haitakufa kamwe.

Huku wakisema kuwa walikuwa wakimshukuru Waziri Mkuu kwa kauli yake, viongozi hao wa DECI walipinga msimamo wa Pinda wa kuuita mchezo wao kuwa ni upatu na uliotawaliwa na ujanja ujanja ambao mwisho wake ni kuwaliza washiriki wake.

Viongozi hao ambao ni wachungaji wa Kanisa la Jesus Trust for Deliverance waliendelea kusisitiza kwamba, DECI ni maono na ufunuo.

“DECI ilianzishwa na kusajiliwa mwaka 2007 kwa kufuata taratibu zote chini ya uasisi wa kanisa hilo…waasisi walikuwa wamepata mzigo na maono ya kushirikiana na serikali katika kupambana na umaskini. Sisi Wakristo tunaamini ukipiga magoti Mungu anakujibu…waasisi hao waliomba si kwa wiki wala miezi, ni muda, wegine wanaona tunajenga hoja ya kudhulumu, lakini sivyo.

“Baada ya kumuomba Mungu kwa kina, wakapata majibu juu ya mateso ya jamii wanamoishi, wakaomba Mungu awafungulie watu wakaunganika na makanisa mengine hata ya nchi jirani, wakajiuliza tufanye nini, na baada ya hapo walianzisha DECI kwa madhumuni mengi na jinsi ya kuwasaidia watu, lakini kwa maono waliyoyapata wakaona ni bora kuanza na ‘Microfinance’, wakajikita katika kupanda na kuvuna, ambako ni lazima iendane na taratibu zinazofahamika,” alisema Kipilimba.

Alisema, wanasikitika wao kama viongozi wa DECI hawajawahi kupata nafasi ya kukaa na serikali, kwani hata walipowatafuta, hawakuwapata kirahisi ingawa leo wamewaita upatu, piramidi na matapeli. Ili kuondoa dhana hiyo na kuweka mambo sawa, wameitaka serikali ikae pamoja nao.

“Kauli ya Waziri Mkuu ni nzuri ingawa sisi tuna hoja ya kupinga kuitwa piramidi, upatu na matapeli, kwa sababu hata mimi nashangaa mtu anayetuita piramidi kwa sababu piramidi haina ‘organization structure’, haina kitu kinaitwa ‘retainer’ ili uweze kupata ‘profit’.

“Sasa tunataka tukae na serikali tuwaonyeshe, watukosoe kwani dhumuni la DECI ni kutumia nguvu na uwezo ili wajasiriamali wadogo waweze kuwa wakubwa na hapo ndipo tunapokabwa tueleze, hatuelezi ng’o.

“Tunaishukuru sana BoT kwa tangazo lake kwani wengine walikuwa wanadhani tunaichukia… BoT tumekuwa tukiwasiliana nayo tangu mwaka 2007 tuliposajili. Biblia ina maneno haya: ‘Tunawarudi tuwapendao’, leo huyu aliyepewa kusimamia, Registrar wa BoT, anaturudi hatuna ugomvi na BoT. Tulipokuwa tunawasiliana na BoT kuna wataalamu walitushauri, kwa hiyo hatuwezi kusema wanatuchukia.

“Sisi tumekuja tuwaeleze washiriki wetu, tuwatie moyo kwa sababu kwenye ule mkutano uliofanyika Viwanja vya Sabasaba kwenye Ukumbi wa PTA hatukuwepo, tunataka tuwatie moyo washiriki wetu kuwa DECI bado inaendelea na mazungumzo na serikali.

“Tume zilizoundwa bado zinapita katika maofisi yetu kutuhoji, hivyo washiriki wetu wawe na subira, wasiwe na hofu, tunaamini serikali inachokifanya ni kizuri tu, hata taarifa za BoT ni nzuri, tunajua wameathirika na kupotoshwa kuwa sisi ni upatu, piramidi, hilo wasijali, tunawaomba wale ambao wamepanda waendelee maana ukipanda mbegu nyingi mavuno ni mengi,” alisema Kipilimba.

Aidha akielezea idadi ya washiriki pamoja na fedha zilizopo, Mwenyekiti wa Bodi ya DECI, Mtaresi, alisema hadi sasa wana washiriki zaidi ya 700,000; fedha zilizopandwa ni sh bilioni 54 na zilizovunwa ni bilioni 38/-.

Alisema hata hivyo kuwa, baada ya kutolewa kwa matangazo ya BoT, zaidi ya sh bilioni tano, zimeng’olewa ili kurejesha fedha hizo kwa waliopanda, hivyo kwa sasa wana sh bilioni 11 ambazo wamezihifadhi benki bila kutaja jina la benki kwa madai kuwa ni siri.

Mwenyekiti huyo alisema, kama DECI kingekuwa chombo hatari, basi wangekuwa wamefikishwa katika vyombo vya sheria, lakini hadi kufikia juzi hakuna mtu yeyote aliyefika polisi kudai kama DECI imemdhulumu au imemfanyia lolote baya.

Aidha alipoulizwa kama chombo hicho kina uhusiano wowote na watu wa kutoka nchi za nje, mwenyekiti huyo aliendelea kusisitiza kuwa wao ndio waasisi, na kwamba hata serikali ifikirie kuwa jambo hilo linafanywa na Watanzania.

“Najua gharama niliyotumia kumlilia Mungu juu ya kuweka chombo hiki, leo DECI imeanzishwa Mabibo, serikali ichunguze hili jambo. Viongozi watupe nafasi, tukikaa tutawaeleza kinachostahili,” alisema.

Alipoulizwa juu ya faida kubwa ambayo anapata mpandaji, Mtaresi alisema anashangaa kuona hata watu wanaojua mahesabu wanahoji juu ya jambo hilo ingawa awali alisema hawako tayari kutoa mfumo wanaotumia.

Pia viongozi hao wa DECI walikanusha kauli zilizopata kutolewa kwamba kampuni hiyo inaua Saccos na kuwafanya watu wasihifadhi pesa zao benki.

“Nia ni kuwafanya washiriki waweze kupata pesa za kwenda kuweka Saccos ili waweze kukopa na kuhusu benki, tulishafanya mipango washiriki wote wakapokelee fedha zao katika mabenki, lakini bado hatujafikia muafaka,” alisema.

Walipoulizwa juu ya barua ambayo BoT inadai kuwa DECI iliomba kufanya shughuli ya kutoa mikopo na si kupanda na kuvuna kama ilivyo sasa, viongozi hao walisema kuwa BoT inawazushia na kwamba walifanya taratibu zote wakimtumia mshauri wao.

“Tuliomba tuwe Microfinance benki tukaambiwa tuandike barua tutajibiwa na hatujajibiwa mpaka leo… na kitengo cha Microfinance cha BoT ndio walezi wetu DECI,” alisema.

Kuhusu usalama wa washiriki, Mtaresi alisema kuwa usalama wanao wa kutosha, lakini akakataa kusema ni upi na kusisitiza kuwa mtu akihitaji kung’oa wanampa na kama mtu akifa zipo taratibu zinazofanyika kurejesha fedha hizo.

Aidha, viongozi hao walisema wanahofia usalama wao kwani tangu kuzuka kwa sakata hilo, mmoja wa viongozi wake, aliwahi kutekwa nyara na watu asiowajua, lakini alifanikiwa kuwatoroka.

“DECI imeathirika si tu kwa wanachama wanaong’oa, bali hata usalama wetu sisi ni hatari... nilitekwa nyara wakaniambia twende kwa fulani (simtaji) ndiye atakayenitatulia tatizo langu, mimi nikasema bila Rais Kikwete wala Waziri Mkuu Pinda na BoT siendi.

“Watu hao walikuwa kwenye Pajero ndogo namba nimezihifadhi, nikawaambia subirini huku nikiomba Mungu anisaidie, niliweza kuwashawishi na kuwatoka,” alisema Kipilimba.

Katika hatua nyingine, DECI imetangaza kufunga ofisi za matawi yake yote nchini hadi hapo itakapomaliza majadiliano na serikali.

Ingawa viongozi wake hawakutoa taarifa hiyo katika mkutano wao na waandishi wa habari, lakini tangazo la kuzifunga ofisi zao, lilisikika kupitia kituo cha Redio WAPO.

Tanzania Daima ilipofika katika ofisi za makao makuu ya DECI, Mabibo, ilishuhudia zikiwa zimefungwa, huku kukiwa na makundi ya watu waliokuwa wakijadili hatma ya kampuni hiyo.

Kati ya watu hao, wapo ambao walikuwa wamekwenda kwa nia ya kuvuna, na wengine wakiwa wanasikilizia hatma yao ambao walisikika wakiilaumu serikali kwa hatua yake ya kutotambua shughuli za DECI.

Kwa upande wake, Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, jijini Dar es Salaam, Zachary Kakobe, aliitaka serikali isiionee huruma DECI kutokana na kukiuka taratibu za nchi.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kanisa hilo, Kakobe aliitaka serikali ichukue hatua haraka.

Kwa maelezo ya Kakobe, fedha hizo zingekuwa benki, wananchi wasingepata hasara, lakini kwa kuwa zilipandwa DECI lazima hasara iwepo.

Kwa upande mwingine, askofu huyo aliwataka viongozi wa siasa wasitafute kura kwa wananchi kwa kuwaruhusu kuvunja sheria, bali wawafundishe kusimama katika sheria.

Monday, April 13, 2009

The most valuable soccer teams


The world's richest clubs are prospering despite the global recession.


The financial crisis has yet to derail the world's most valuable soccer teams. Our calculations show the top 25 teams are now worth, on average, $597 million, 8% more than the previous year.
These clubs posted operating income (in the sense of earnings before interest, taxes, depreciation and amortization) of $42 million during the 2007-2008 season, 20% more than the top 25 clubs earned the previous year. There are now five clubs (Manchester United, Real Madrid, Arsenal, Bayern Munich and Liverpool) worth at least $1 billion. Only the National Football League has more billion-dollar teams (19).


"The value [of European soccer] is still there," says sports banker Robert J. Tilliss, founder of Inner Circle Sports. "The demand from broadcasters and sponsors has continued to rise."


One reason most top clubs have continued to see revenue increases and post strong profits is that they have lucrative multi-year broadcasting and sponsorship deals that have not been affected by the recession.


BSkyB, owned by News Corp. ( NWS - news - people ), and Setanta pay out roughly $1.8 billion a year for Premier League rights. Arsenal, Liverpool and Schalke 04 have multi-year deals with Emirates, Carlsberg and Gazprom that pay these clubs over $15 million a season.


More than half of the 20 clubs with the highest revenue signed current uniform sponsors within the last two years. The deals are good through 2013, on average, protecting teams' biggest source of sponsorship revenue (along with stadium-naming rights).


On the broadcast side, German, English and the top Spanish clubs all have deals in place through 2014, with French rights due for renegotiation in 2012 and Italy set to return to centrally sold rights in 2010, according to a report by the Sports Business Group at Deloitte.


Burnished by that relative stability and by the sport's growing popularity throughout China and Southeast Asia, big-ticket investors have continued to pour money into England's Premier league. The biggest splash in the last year: The sale of Manchester City to Sheikh Mansour Bin Zayed Al Nahyan for nearly $385 million.


If anything demonstrates the value premium Premier League clubs enjoy it is Man City selling for a multiple of revenue (2.4 times) in line with our estimates for Bayern Munich and Real Madrid. Man City does not own City of Manchester Stadium, where it plays, and despite settlement of its debts and huge spending on players (nearly $150 million) by the Sheikh, we estimate he overpaid by 25% for a money-losing toy.


With its capitalistic bent, European soccer rewards the best-performing clubs with higher broadcasting revenue. Leading the charge is the world's most valuable sports franchise: England's Manchester United, worth $1.87 billion.


With $160 million in operating income, ManU was also the most profitable team. A big assist: $68 million in Champions League distributions after winning Europe's top competition last year.


The real value in ManU is its Old Trafford stadium (capacity: 76,000--27% bigger than the next-biggest in England). With star strikers Wayne Rooney and Cristiano Ronaldo keeping the stadium packed, Old Trafford raked in over $200 million in ticket and concessions revenue last season, more than any other team.


The second spot went to Spanish heavyweight Real Madrid, worth $1.35 billion. The team has continued to shine on the pitch despite the departure of superstars David Beckham, Zidane and Ronaldo during the past two years.


The Whites ended the 2007-2008 campaign as the highest-scoring (84 goals) and the least-scored-upon (36) team in its league and set a new La Liga record by notching 85 points, 18 more than third-place Barcelona. The second season of a $1.4 billion rights deal with broadcast partner Mediapro generated $576 million in revenue for the team, more than any other sports franchise.
Clubs with piles of debt have not been immune to the credit crunch. English football authorities, in particular, have sounded alarms about more than $4.5 billion of debt on the books of Premier League teams. Liverpool, the third-most valuable U.K. team, had roughly $600 million of debt outstanding at fiscal year-end in June 2008 thanks to a $314 million leveraged buyout by American businessmen Thomas O. Hicks and George Gillett.


A looming deadline to repay or refinance a related bank loan arrives in July, and should credit markets remain tight through the summer, the owners could be faced with a choice between default and selling the club at a discount.


Falling out of the top 25 were Spanish club Valencia and England's West Ham United, which, despite middle-of-the-pack finishes in recent years, has been limited by its diminutive Boleyn Ground stadium with room for just 35,647 fans. Spain's Valencia has suffered from a massive debt load used to finance player costs and a new 75,000-seat stadium that could add 50% to the former stadium's capacity at a time when the team has struggled to finish in the top half of Spain's Primera Liga.


Rejoining the list this season was Scotland's Glasgow Rangers, and joining for the first time was VfB Stuttgart from Germany. Dark horse Stuttgart won Germany's Bundesliga championship in '07, qualifying it for the Champions League last year--a windfall allowing for plans to improve its Mercedes-Benz Arena.


As for Scottish Premier League team, the 'Gers had an historic run to the UEFA Cup final against Russian side Zenit St. Petersburg. Improvements to home field Ibrox Park have followed and could mean bigger profits down the road.

Saturday, April 11, 2009

AMANI;ITADUMU?


Mojawapo ya mambo ambayo tunajivunia kama watanzania ni kuwa miongoni mwa nchi chache sana za kiafrika ambazo mpaka hivi leo viongozi wa upinzani na wale wa chama tawala hukutana pamoja,wakala,wakacheka na wakajumuika katika mambo mbalimbali ambayo yana mvuto au muelekeo wa kitaifa. Hapo sera huwekwa pembeni.Taifa kwanza.

Hili ni suala ambalo hatuna budi kujivunia…japo hilo basi.Wasiwasi nilionao ni kama amani hii,furaha hii,vicheko hivi vitadumu kwa muda gani.Nasema hivyo kwa sababu pamoja na vicheko,mwananchi wa kawaida bado anaumia.Bado anateseka.Hajaona faida wala matunda ya uhuru.Mpaka leo hii hata huo umeme unaogonga vichwa katika vyombo vya habari na mitaani yeye haujui.Hajawahi kutumia umeme! Kula yake ni ya kubahatisha.Pengo kati ya walionacho(mara nyingi kwa njia zisizo halali aka ufisadi) limekuwa kubwa kuliko Ngorongoro yetu.Hilo ni tatizo.Lapasa limkoseshe mtu usingizi.

Tunapocheka,tunapofurahi na tunapokumbushana kwamba tuna amani ni lazima tumkumbuke mwananchi…yule ambaye husahaulika magazetini,wilayani,mikoani na hata Bungeni. Tukifanya hivyo,tutakuwa na kila sababu ya kufurahi…kufurahi kwa pamoja! Vinginevyo…bora kununa

KILI MUSIC AWARDS WINNERS ARE…


Hatimaye zile tuzo za Kili Music zilifikia kilele chake hapo jana ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar-es-salaam.

Washindi walikuwa kama wafuatao;

1.Mwimbaji Bora wa Kike- Keisha(pichani)
2.Mwimbaji Bora wa Kiume- Mb Dogg
3.Albamu Bora ya Taarab- VIP( Jahazi Modern Taarab)
4.Wimbo Bora wa Taarab- VIP(Jahazi Modern Taarab)
5.Wimbo Bora wa Mwaka- Anita (Matonya ft Lady JayDee)
6.Wimbo Bora wa Kiswahili- Heshima kwa Mwanamke (FM Academia)
7.Albamu Bora ya Kiswahili- Pekecha Pekecha(Akudo Impact)
8.Wimbo Bora wa R& B- Natamani (Q Jay ft Makamua & Joslin)
9.Albamu Bora ya Muziki Asilia- Dela Dela( Che Mundugwao)
10.Wimbo Bora wa Hip Hop- Ngoma Itambae(Chid Benz)
11.Wimbo Bora wa Reggae- Ripoti (Tunda Man)
12.Msanii Bora wa Rap- Mangwea
13.Wimbo Bora wa Afrika Mashariki- Salary(Nameless from Kenya)
14.Mtunzi Bora wa Muziki- Karama Legesu
15.Mtayarishaji Bora wa Muziki- Hammie B
16.Mwandikaji Bora wa Muziki- Prof.Jay
17.Wimbo Bora wa Zouk- Nalivua Pendo(Mwasiti)
18.Mtayarishaji Bora wa Video- Kallaghe Production
19.Wimbo Bora wa Collaboration- Anita (Matonya ft Lady Jaydee)
20Wimbo Bora wa Asilia- Kazi ya Dukani(Dogo Mfaume)
Kwa habari na picha zaidi za tukio hili unaweza kutembelea hapa na hapa. Je uliodhani wangeshinda ndio walioshinda?Nini ushauri wako kwa kamati ya Kili Awards ili kuboresha zaidi hapo mwakani? Ukitaka kujua washindi walikuwa wakishindana na nani katika category zao bonyeza hapa. MK inawapongeza washindi wote.

CLUB RAHA LEO SHOW NA UNCLE J!


Yapo mambo ambayo ukijaribu kuyakumbuka bila shaka unaweza kutokwa na machozi.Yaweza kuwa machozi ya furaha na pia yaweza kuwa ya huzuni.Lakini kama wasemavyo walimwengu,yote huwa ni sehemu ya maisha.

Mojawapo ya mambo ambayo nikiyakumbuka huwa napata gunia la hisia tofauti tofauti ni kipindi cha Club Raha Leo Show cha enzi hizo za Radio Tanzania Dar-es-salaam kilichokuwa kikiendeshwa na Julius Nyaisangah au maarufu kama Uncle J(pichani). Hizo ni zile enzi za utawala wa RTD kabla vituo mbalimbali vya FM havijaanza kufumuka ili kutanua wigo wa habari na mawasiliano na pia kuongeza ushindani kama sio kutuibulia pia DJs wengine ambao nao wana nafasi ya pekee katika historia ya utangazaji nchini akiwemo rafiki yangu Mike Mhagama na wengine wengi.

Kipindi cha Club Raha Leo Show kilikuwa ni sehemu muhimu sana kwa wasanii na bendi kutambulisha nyimbo zao,kukutana na mashabiki wao na pia nafasi nzuri ya wasikilizaji kutuma na kupokea salamu.Sina uhakika kama kipindi hiki bado kinaendelea.Lakini kama hakipo tena swali muhimu ni kwanini hakipo?

Kwa ijumaa ya leo burudani nzima inatoka hapo Club Raha Leo Show.Hapo utamsikia Uncle J akishirikiana na mtangazaji mwingine mahiri,Michael Katembo. Bendi iliyopo studio ni wana-Ndekule.Bila shaka kipindi hiki kitakukumbusha mbali.Natumaini utacheka kwa furaha na kama ikitokea ukalia,basi natumaini yatakuwa machozi ya furaha,

Thursday, April 2, 2009

Enzi zile alipoanza kutambulika rasmi ilitokana na wimbo wake uliokwenda kwa jina “Nipo Bize”.Si unakumbuka jinsi alivyokuwa akimwambia kimwana wake k


Enzi zile alipoanza kutambulika rasmi ilitokana na wimbo wake uliokwenda kwa jina “Nipo Bize”.Si unakumbuka jinsi alivyokuwa akimwambia kimwana wake kwamba asimtafute kwa sababu yuko bize?

Basi yawezekana ni kweli kwamba mshkaji huwa yuko bize kwani Jafarai ameshakamilisha albamu yake mpya itakayokwenda kwa jina Wali Nazi. Albamu hiyo itakuwa na nyimbo 9 ambazo zote zimerekodiwa katika studio za Fish Club za jijini Dar.Katika albamu hiyo Jafarai amewashirikisha wasanii wengine kama vile mwanadada Naazizi kutoka Kenya,Lamar ambaye pia ni producer wa albamu hiyo na pia Wateule.

Mojawapo ya nyimbo zilizomo katika albamu hiyo ni wimbo ambao unatamba katika vituo mbalimbali vya redio hivi sasa.Wimbo unaitwa Napenda Nini .Katika wimbo huu Jafarai ameshirikiana na mwanadada Fatma. Ni wimbo ambao una tungo kali,matata na ambayo nadhani ni huru kusema unaweza kuitafsiri unavyotaka wewe.Ni kazi nzuri ya sanaa ambayo inaonyesha jinsi gani lugha ya Kiswahili ni pana.